Date: 
14-09-2024
Reading: 
Hagai 1:12-15

Jumamosi asubuhi tarehe 14.09.2024

Hagai 1:12-15

12 Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana.

13 Ndipo Hagai mjumbe wa Bwana, katika ujumbe wa Bwana, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema Bwana.

14 Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao;

15 katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa Dario mfalme

Uwakili wetu kwa Mungu;

Baada ya kuona watu hawamjengei Mungu nyumba, Bwana alimtuma Hagai kuleta ujumbe huu;

Hagai 1:5-8

5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.

Sasa somo tulilosoma asubuhi ya leo, ni wito wa Zerubabeli na wenzake wakiitika kuijenga nyumba ya Bwana. Ujumbe wa Hagai uliwafanya waogope mbele za Bwana, wote wakajumuika kuijenga nyumba. Tukikumbuka neema ya Bwana kwetu, tunawajibika kumtumikia siku zote za maisha yetu. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa