MATANGAZO YA USHARIKA 

TAREHE 02 JUNI, 2024

SIKU YA BWANA YA 1 BAADA YA UTATU

NENO LINALOTUONGOZA NI

CHAGUENI MTAKAYEMTUMIKIA 

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 26/05/2024

4. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Leo tarehe 02/06/2024 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibuni.

7. Uongozi wa usharika unapenda kuwakumbusha washarika wote walioahidi sadaka za mavuno, na kuchukua vitu vya mnada katika mavuno ya mwaka 2022-2023 kumalizia nadhili zao walizojiwekea mbele za Mungu.

8. Jumamosi ijayo tarehe 08/06/2024 kutakuwa na mtihani kwa watoto wa Kipaimara mwaka pili. Mtihani huu umeandaliwa na Dayosisi ngazi ya kwanza. Hivyo tunaomba Ushirikiano wenu Wazazi na Walezi watoto wafike kwa wakati.

9. Watoto wa Shule ya jumapili wataanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Mikaeli jumamosi ijayo tarehe 08/06/2024 Kingereza wataanza saa 3.00 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana na Kiswahili wataanza saa 6.00 mchana mpaka saa 8.00 mchana.

10. Kitenge chetu cha kiharaka kinapatikana kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya shilingi 40,000/= 

11.  NDOA: NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA TUNATANGAZA NDOA YA TAREHE 22/06/2024 SAA 9.00 ALASIRI KATI YA

  • Bw. Anania Wilbad Mkota na Bi. Annamaria Amon Mwambela

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 08/06/2024. SAA 10.00 JIONI KATI YA

  • Bw. Joseph Peter Moshi na Bi. Joyce Joseph Davidson

NDOA HII IFUATAYO ITAFUNGWA KKKT ISHARIKA WA KANISA KUU (KENGELE TATU) BUKOBA, KAGERA KATI YA

  • Bw. Joshua Yoshua Justus na Bi. Prisca Christian Ngaiza

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

12. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Upanga: kwa Bwana na Bibi William Sabaya
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Lwaga
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Shanny Mbogolo
  • Kinondoni: Kwa ……………………………
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Mcharo Mlaki
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa ………………..
  • Ilala, Chang’ombe, Buguruni: Kwa Mama Itemba
  • Oysterbay, Masaki: Kwa …………………….

13. Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo ye

tu, Bwana ayabariki.