Date: 
12-12-2023
Reading: 
Ufunuo 22:6-9

Jumanne asubuhi tarehe 12.12.2023

Ufunuo wa Yohana 22:6-9

6 Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.

7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.

8 Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo.

9 Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.

Yesu anakuja katika Utukufu wake;

Yohana alifunuliwa mbingu mpya iliyoandaliwa kwa ajili ya wateule. Katika kufunuliwa huko anatumwa kuleta ujumbe wa Bwana, kwamba anakuja upesi. Yohana katika ufunuo huo anakiri kumuona Bwana nakumsujudia.

Ukisoma zaidi unaona Yohana akitumwa kusema;

Ufunuo wa Yohana 22:12-14

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

Ujumbe wa asubuhi ya leo ni kuwa Bwana anakuja. Bwana anapokuja anatujia sisi tulio watu wake. Anakaa kwetu. Kuja kwa Bwana kwetu ni kwa daima. Hivyo mruhusu akae kwako, ukijiandaa kumpokea tena atakaporudi kwa mara ya pili. Amina.

Siku njema.

Heri Buberwa