Date: 
19-08-2023
Reading: 
Luka 19:41-44

Jumamosi asubuhi tarehe 19.08.2023

Luka 19:41-44

41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,

42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.

43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.

Mithali 14:34

Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Yesu aliwatuma wanafunzi wawili kwenda kijiji cha karibu kumletea mwanapunda. Walimleta huyo mwanapunda ambaye Yesu alimpanda akaingia Yerusalemu kwa shangwe. Ujumbe tuliousoma ni maneno aliyoyatamka Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu, kwamba hawakumpokea. Lakini aliwaita kutambua kuwa alikuwa akiwajia, hivyo wampokee yeye aliye Mwokozi wa Ulimwengu 

Kuingia Yerusalemu kwa Yesu ilikuwa ni hatua ya kuiendea njia ya mateso, kifo hadi kufufuka. Na baada ya kufufuka kwake, alishinda dhambi na mauti ili sisi tuokolewe. Wajibu wetu ni kuendelea kudumu katika wokovu tukienda haki kwa Utukufu wa Mungu. Amina.

Jumamosi njema 

 

Heri Buberwa