Date: 
20-07-2023
Reading: 
1 Petro 3:8-9

Alhamisi asubuhi tarehe 20.07.2023

1 Petro 3:8-9

8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;

9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

Amri ya Upendo;

Petro katika waraka wake kwa Kanisa anaandika juu ya watu kuzingatia matendo yafaayo watu wanapokaa pamoja. Anafundisha juu ya familia, yaani wake kuwatii waume zao, waume kuwapenda wake zao, na wengine wote kutimiza wajibu wao kama alivyoagiza Kristo. Na mwisho katika somo la asubuhi ya leo ndipo anasema watu wote tuhurumiane na kupendana pasipo kulipa baya kwa baya.

Asubuhi hii tunaalikwa kuishi tukitimiza wajibu, kila mmoja kwa nafasi yake. Tutende yote inavyostahili kwa uaminifu tukihurumiana na kupendana kama lilivyo agizo takatifu la Mungu wetu.

Tuache mabaya, tutende mema, tupendane. Amina.

Alhamisi njema.

 

Heri Buberwa