Date: 
10-01-2023
Reading: 
Marko 1:9-11

Jumanne asubuhi tarehe10.01.2023

Marko 1:9-11

[9] Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. [10]Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; [11]na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe. Ubatizo wetu; Marko 1:9-11 [9] Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. [10]Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; [11]na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

Ubatizo wetu;

Marko anaeleza kwa ufupi kuhusu ubatizo wa Yesu, kwamba Yohana alimbatiza Yesu mbingu zikapasuka, Roho akamshukia Yesu na Mungu akamtambulisha Yesu kama mwanae. Ulikuwa ubatizo wa toba, lakini Yesu alibatizwa ubatizo huo siyo kwa sababu alikuwa na dhambi, bali ilipaswa kuwa hivyo kwa sababu alikuwa anaanza huduma yake. Baada ya ubatizo ule Yesu alitambulishwa kama Mwana wa Mungu, na Mwokozi wa ulimwengu. Yesu huyu ndiye tuliyempokea tulipobatizwa. Tunapokaa katika ubatizo huu tunamtangaza Kristo aliye Mwokozi wetu, pia tunakuwa na uhakika wa uzima wa milele, maana ubatizo ni wokovu kamili. Unaiishi ahadi ya Ubatizo?

Siku njema.