Date: 
03-09-2022
Reading: 
Hesabu 9:15-23

Jumamosi asubuhi 03.09.2022

Hesabu 9:15-23

[15]Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi.

[16]Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku.

[17]Na kila lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao.

[18]Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao.

[19]Na lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, ndipo wana wa Israeli walipolinda malinzi ya BWANA, wala hawakusafiri.

[20]Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri.

[21]Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri.

[22]Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri;

[23]bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; wakayalinda malinzi ya BWANA, kwa mkono wa Musa.

Iweni wanyenyekevu 

Kwa sehemu tuliyosoma, Israeli waliposafiri kuelekea nchi ya ahadi chini ya Musa waliongozwa na wingu lililokuwa mfano wa moto. Lilipoinuliwa walisafiri na lilipokaa hawakusafiri. Waliongozwa na amri ya Bwana kusafiri chini ya kwa mkono wa Musa.

Tunachokiona leo asubuhi ni Israeli kuongozwa na wingu. Lakini wingu hili lilitoka kwa Bwana. 

Kumbe nasi tunahitaji kuongozwa na Bwana katika maisha yetu. Tusitumie akili zetu, bali tunyenyekee kwake ili atuwezeshe kumtumikia kwa ukamilifu na kuurithi uzima wa milele.

Jumamosi njema