Date: 
31-05-2022
Reading: 
2Wafalme 20:1-11

Jumanne asubuhi 31.05.2022

2 Wafalme 20:1-11

1 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,

3 Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

4 Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,

5 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.

6 Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.

7 Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.

8 Hezekia akamwambia Isaya, Je! Kutakuwa na ishara gani ya kwamba Bwana ataniponya, nami siku ya tatu nitapanda nyumbani kwa Bwana.

9 Isaya akamwambia, Jambo hili litakuwa ishara kwako, itokayo kwa Bwana, ya kwamba Bwana atalifanya neno hilo alilolinena; je! Kivuli kiendelee madaraja kumi, au kirudi nyuma madaraja kumi?

10 Hezekia akajibu, Ni jambo jepesi kivuli kuendelea madaraja kumi; la, hicho kivuli na kirudi nyuma madaraja kumi.

11 Isaya nabii akamlilia Bwana; akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, ambayo kilikuwa kimeshuka katika madaraja ya Ahazi.

Sikia kuomba kwetu;

Hezekia alikuwa afe, lakini ujumbe toka kwa Bwana kupitia kwa Isaya ulisababisha afanye sala, Mungu akamponya. Kilichomponya Hezekia ni kumsikiliza Isaya, akamtii Mungu akiomba kwa imani na Mungu akamponya.

Neno la Mungu linatuelekeza kuomba kwa imani. Tunaalikwa kuwa watii kwa neno la Mungu, tukienda mbele za Mungu wetu kwa imani na unyenyekevu, pale tunapomkosea. Ukikosa tubu. Mungu yuko tayari kukusikia.

Siku njema.