Date: 
01-08-2022
Reading: 
Mwanzo 40:1-6

Jumatatu asubuhi tarehe 01.08.2022

Mwanzo 40:1-6

[1]Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri.

[2]Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji.

[3]Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu.

[4]Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo.

[5]Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani.

[6]Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika.

Mungu amejaa neema inayotuwezesha;

Mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu katika Misri walimkosea Bwana wao, akawaghadhabikia maakida wake hao na kuwatia gerezani walikokutana na Yusufu. Bila shaka kuna mambo hayakwenda sawa kwenye kazi zao, ndiyo maana Mfalme alichukia. Yusufu alikaa nao karibu mle gerezani, bila shaka kwa kuwa alikuwa mwenyeji wao kwenye gereza lile.

Zipo nyakati ambazo tunapitia magumu katika kazi zetu. Wakati mwingine tunakosea sana kiasi cha kupoteza kila kitu, yaani hata kazi. Tunajiona tuko kifungoni hata kama tuko huru. Ni wito wangu kukaa kwa Yesu wakati wote, katika shida yoyote, mahali popote, maana Mungu amejaa neema inayotuwezesha.

Wiki njema.