Jumamosi asubuhi tarehe 11.02.2023
Matendo ya Mitume 11:19-26
19 Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano, wakasafiri hata Foinike na Kipro na Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao.
20 Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kiyunani, wakihubiri habari njema za Bwana Yesu.
21 Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.
22 Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.
23 Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.
24 Maana alikuwa mtu mwema amejaa Roho Mtakatifu na imani; watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana.
25 Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;
26 hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.
Tunaokolewa kwa neema;
Leo asubuhi tunaona Injili ilivyohubiriwa hata baada ya Stefano kufa. Injili ilihubiriwa hadi Yerusalemu. Barnaba naye alihubiri akihimiza umoja katika Kristo, baada ya kuiona meema ya Mungu. Alitambua neema ya Mungu kuwaokoa watu, ndiyo maana akawasihi kuwa wamoja wakiambatana katika Bwana.
Ndani ya Antiokia Barnaba na wenzake walihubiri Injili, na ndani ya mwaka mzima Kanisa likawepo Antiokia. Mitume wanaonekana kuhubiri Injili na watu kumwamini na kumpokea Yesu. Yesu huyu ndiye aliyetuokoa, ambaye asubuhi hii tunakumbushwa kudumu katika yeye ili neema yake isiondoke kwetu.
Jumamosi njema.
Heri Buberwa