MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 JANUARI, 2022

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

MUNGU ANAONDOA UBAGUZI

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti.

3. Matoleo ya Tarehe 16/01/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu pamoja na Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.30 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Mafundisho ya Kipaimara Mwaka wa Kwanza na wa pili kwa lugha ya Kiswahili yataanza jumamosi ijayo tarehe 29/01/2022 saa 3.00 asubuhi. Kwa darasa la Kingereza Mwaka wa pili nao wataanza jumamosi ijayo tarehe 29/01/2022 saa 4.30 asubuhi. Pia darasa la Kingereza kwa mwaka wa kwanza wataanza jumamosi ya tarehe 05/02/2022 saa 3.00 asubuhi. Wazazi na Walezi mnaombwa kuwahimiza watoto wafike darasani na kwa Wakati uliopangwa.

6. Umoja wa vijana idara ya Uinjilisti inapenda kuwatangazia vijana wote hapa usharikani kuwa kutakuwa na mtihani wa Biblia Tarehe 12/03/2022. Hivyo wanaomba vijana watakao kuwa tayari kushiriki mtihani huo wajiandkikishe majina yao kwa viongozi wa Umoja wa vijana. Maandalizi ya mtihani yataanza jumatano tarehe 26/01/2022. Vijana wote mnakaribishwa.

7. Familia ya Bwana na Bibi Kennedy Kenan Lyova wamepata zawadi ya mtoto wa kike tarehe 17/01/2022 katika hospitali ya Masana. Baba, Mama na mtoto wanaendelea vizuri.                         

8. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 30/01/2022 

IBADA YA KWANZA

Walimu wa Shule ya Jumapili watamshukuru Mungu kwa kuwasaidia katika huduma ya kufundisha watoto 2021 na kuwapa kibali cha kuingia mwaka 2022.

Neno: Zaburi 100:1-3, Wimbo: 264 fungu la 1 -2

IBADA YA PILI

Sospert Muro atamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyomtendea ikiwa ni pamoja na kumvusha salama mwaka 2021.

Neno: Zaburi 118:1-5, Wimbo: Kwaya Kuu(kimbilio langu)

9. Washarika ambao hawapo kwenye group whatsap ya Usharika kwa ajili ya kupata taarifa za usharika, wafike ofisini ili kuandika namba zao waweze kuingizwa kwenye group.

10. NDOA.

Matangazo ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo karibu na duka letu la vitabu.

11. Zamu: Zamu za wazee leo ni Kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.