MATANGAZO YA USHARIKA TAREHE 9 JUNI, 2019
SIKU YA PENTEKOSTE
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
ROHO NDIO MSAADA WETU
- Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
- Wageni: Hakuna mgeni aliyefika na cheti.
- Alhamisi ijayo tarehe 13/06/2019 saa 11.30 jioni kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi. Karibu utupate akili na hekima ya kumjua Mungu. Usikose.
- Uongozi wa Usharika unaendelea kuwakaribisha wote kwenye ibada nzuri zinazofanyika kila siku katikati ya wiki hapa usharikani, ibada ya Morning Glory inayoanza saa 12.00 – 1.00 asubuhi, siku ya Jumatatu hadi Ijumaa, ambayo hukupa fursa ya kuanza kazi na uwepo wa Mungu. Ibada ya Mchana kila siku saa 7.00 – 7.30 mchana ambayo inakupa nafasi ya kupata faragha binafsi na Mungu. Wote mnakaribishwa.
- Kesho Jumatatu tarehe 10/06/2019 saa 11.00 jioni Kutakuwa na ibada ya kuenea kwa Roho Mtakatifu. Kwaya zote zitahudumu. Zamu za wazee itakuwa ni kundi la kwanza.
- Jumapili ijayo tarehe 16/06/2019 ni siku yetu Maalum ya Harambee ya Kiharaka. Ibada zitakuwa mbili kama kawaida. Ya kwanza itaanza saa 1.00 asubuhi na ya pili itaanza saa 4.00 asubuhi. Washarika tuiombee siku hiyo. Aidha Vitenge vya Kiharaka vipo kwa bei ya sh. 10,000/=. Vitenge hivi ndiyo sare siku ya Harambee kwa Washarika wote.
- NDOA
NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa za tarehe 29.06.2019
SAA 7.00 MCHANA
Bw. Mussa Mayala Masala na Bi. Maryrose Jacob Mtei
SAA 10.00 JIONI
Bw. Baraka Adon Francis na Bi. Brenda Joseh Korassa
Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa za tarehe 22.06.2019.
SAA 9.00 ALASIRI
Bw. Richard Absalum Mpogole na Bi. Janeth Daniel Mgaliwa
Ndoa hii ifuatayo itafungwa KKKT Kanisa Kuu Njombe kati ya
Bw. Ephrahim Yohana Sanga na Bi. Neema Aston Kibona
Matangazo mengine ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao matangazo.Karibu na duka letu la vitabu
- IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
Wazo/Tegeta/Kunduchi/Bahari Beach/Ununio: Kwa Bwana na Bibi Kevela
Mwenge/Kijitonyama/Makumbusho/Sinza/Ubungo/Makongo: Kwa Bi. Mary Kinisa
Mjini kati: Kwa mama Mongi
Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Kwa Dr. na Bibi D. Ruhago
Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi T. Msangi
Tabata: Kwa Bwana na Bibi J. Mwakasege
Oysterbay/Masaki:
Upanga: kwa Bwana na Bibi Nkya – (Mariki Road)
Kinondoni: Kwa Prof. G. Mmari
Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.