MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 03 JUNI, 2018

SOMO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI MUNGU AU ULIMWENGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Wageni waliotufikia na cheti ni

3. Kuanzia jumatatu tarehe 04/06/2018 katika ibada za Morning Glory tutakuwa na Mch. Daniel Mgogo kutoka Mbeya.  Aidha  Alhamisi ijayo tarehe 07/06/2018 kutakuwa na kipindi cha maombi na maombezi yatakayoanza saa 11.30 jioni. Mwalimu atakuwa ni Mwinjilist Baraka Mbise kutoka KKKT Ubungo. Wote mnakaribishwa.

4. Leo tutamtolea Mungu fungu la kumi. 

5. Jumapili ijayo tarehe 10/06/2018 kutakuwa na ubatizo wa watoto na kurudi kundini. Watakaohitaji huduma hii wafike ofisini kwa Mchungaji.

6. Jumapili ijayo tarehe 10/06/2018 familia tatu zitamtolea Mungu shukrani:

7. Katika ibada ya kwanza saa 1.00 asubuhi familia ya Dr. Samuel na Dr. Jennifer Swai watamtolea  Mungu shukrani ya pekee kwa mambo mengi mema aliyowatendea.  Wanaomba washarika tuwasindikize.

Neno: Zaburi 119:65, Zaburi 111: 1-2,  Wimbo: TMW. 262 (Tumshukuru Mungu).

 

Katika ibada ya pili saa 3.30 asubuhi familia ya Mama Helga Israel Laiser wanapenda kumtolea Mungu shukrani kwa mambo mengi mema aliyowatendea, ikiwa ni pamoja na kuwatia nguvu tangu Mzee Israel Kayan Laisser  alipotwaliwa na Bwana miaka kumi iliyopita na Samwel Israel Laisser aliyetwaliwa na Bwana miaka mitatu iliyopita.

Neno: Zaburi 71:1-5, Wimbo: TMW. 255

Pia Katika ibada ya pili familia ya Bwana Davis na Dkt Ellen Senkoro watamshukuru Mungu kipekee kwa Baraka na neema za Mungu alizowatendea.

8. Tarehe 09/06/2018 saa 3.00 asubuhi kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wapya wa Wajane na Wagane. Wajumbe wote wanaombwa wafike bila kukosa.

 

9. Tarehe 06/06/2018 kutakuwa na ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa wanawake kidayosisi utakaofanyika Mkuza. Wanawake wote wanaombwa kufika huko saa 5 asubuhi.  Atakayefungua mkutano huo ni Baba Askofu Alex G. Malasusa. Wanawake wote mnaombwa kuhudhuria.

 

10. NDOA.

Matangazo ya ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba   

  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Rason Mduma
  • Kinondoni: Kwa Profesa G. Mmari
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni:  Watatangaza
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Dr na Mama Rumishaeli Shoo
  • Oysterbay/Masaki: Famila ya Balozi Mangu
  • Mjini kati:  Kwa Mama  Victoria Mwansasu
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Sangiwa
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Kwa Bwana Frank na Bibi Veronica Korassa.
  • Tabata:  Watatangaza

Zamu: Zamu za wazee ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.