MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 16 APRILI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU AMEFUFUKA, HALELUYA!

 1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
 1. Wageni:  Hakuna wageni waliotufikia na cheti.
 1. Leo jioni hatutakuwa na Kipindi cha maombi na maombezi. Kipindi kitaanza tena alhamisi tarehe 20 Aprili kitakachoongozwa na Mtumishi Mbise toka KKKT Ubungo.
 1. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kuwa tamasha la uimbaji ni tarehe 13.05.2017 mazoezi yanaendelea kila Jumatano saa 10.00 jioni. Tunaomba wanawake wa vikundi vyote tuungane pamoja kwa ajili ya maandalizi hayo aidha jumatatu ya pasaka kesho ni siku ya tembea na Kristo,  hivyo wanawake wote Dayosisi watakutana KKKT Kijichi kwa ajili ya kuazimisha Pasaka. Tunaomba wanawake wote tukimaliza ibada hapa usharikani tutaondoka pamoja kwenda kijichi. Sare ni Kitenge cha Dayosisi na mtandio.
 1. Uongozi wa shule ya jumapili unapenda kuwaomba wazazi kuwaleta watoto kila siku ya jumamosi saa 9.00 alasiri ili waanze mazoezi ya nyimbo kwa ajili ya tamasha lao. Mungu awabariki.
 1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya uongozi wa Usharika unapenda kuwatangazia washarika kuwa kuanzia jumapili ijayo tarehe 23/04/2017  hadi tarehe 30/04/2017 kutakuwa na semina ya ndoa itakayofundishwa na Mchungaji Mathias Mushi toka KKKT Arusha. Washarika mnaombwa kuiombea semina hii.  Wote mnakaribishwa.
 1. Jumapili ijayo tarehe 23.04.2017 katika ibada ya pili 3.30 asubuhi familia ya Bwana na Bibi Joseph Mpuya watamshukuru Mungu kwa mema mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na Baraka ya kupata mtoto. Wameomba neno toka

Neno: Zaburi 9:1, Wimbo: Zawadi gani toka Kwaya ya Vijana

 1. Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane wa Azania front utafanyika siku ya jumamosi tarehe 22/04/2017. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria.  Mkutano utaanza saa 3.00 asubuhi.

 

 1. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa  za tarehe 06/05/2017

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Morries Walter Shangali         na     Bi. Elke Norah Sumari

 

SAA 10.00 JIONI

Bw. Eliah Emmanuel Kinyunyu      na     Bi. Emilia Bonifas Mdamba

 

Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa  za tarehe 29/04/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Edson Kakulu Ndanguzi          na     Bi. Gloria Nomsa Labarani

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

 1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba
 • Upanga: Watatangaziana
 • Kinondoni:  Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki
 • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Watatangaziana
 • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Kwa Bwana na Bibi Theophilus Mlaki
 • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
 • Tabata: Watatangaziana
 • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana
 • Mjini kati: Watatangaziana
 • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Bwana na Bibi Mlagha

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.