Date: 
01-06-2022
Reading: 
Luka 11:5-8

Jumatano asubuhi 01.06.2022

Luka 11:5-8
5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,
6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;
7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?
8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.

Sikia kuomba kwetu;

Yesu anatoa mfano wa mtu aendaye kwa rafiki yake kuomba usiku asipewe aombacho. Yesu anasema kwa vile aombavyo bila kuchoka asiondoke, atapewa aombacho na rafiki yake huyo hata kama ni usiku.

Huyu tuliyemsoma anaomba usiku bila kuchoka. Kumbe Yesu anatufundisha kuomba bila kuchoka. Tunapoomba tusichoke. Sala iwe ni maisha yetu, maana ni hakika kuwa  tukiomba tunapewa haja zetu.


Siku njema.