Wanakwaya wa Kwaya ya Agape ya Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ambayo huimba katika ibada ya kwanza (saa moja asubuhi) siku za Jumapili, hivi karibuni walitembelea kitengo cha watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ziara hiyo ilifanyika tarehe 4/2/2022 ambapo kwaya hiyo iliweza kutoa kadi za bima ya afya kwa watoto wahitaji wapatao 64 na pia walitoa mahitaji mbalimbali kama nguo, sabuni, mafuta ya kupaka, miswaki, dawa za meno na vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaopatiwa huduma za kitabibu hospitalini hapo.
Uongozi wa Kwaya ya Agape unapenda kuwashukuru washarika wote waliotoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo ambalo limeleta tabasamu kwenye nyuso za watoto pale hospitalini.
--------------------------------------------
Matukio katika picha wakati kwaya ya Agape ya Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral ilipozuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kutoa zawadi na kuwapa mkono wa Faraja watoto wenye uhitaji wanaopatiwa matibabu hospitalini hapo.
Ripoti hii imeandaliwa na Jane Mhina.