Date: 
06-12-2022
Reading: 
Isaya 24:16-23

Hii ni Advent 

Jumanne asubuhi 06.12.2022

Isaya 24:16-23

16 Toka pande za mwisho wa dunia tumesikia nyimbo, Atukuzwe mwenye haki. Ndipo niliposema, Kukonda kwangu! Kukonda kwangu! Ole wangu! Watenda hila wametenda hila, naam, watendao hila wametenda hila sana.

17 Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani.

18 Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika.

19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.

20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.

21 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia;

22 nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.

23 Ndipo mwezi utatahayari, na jua litaona haya; kwa kuwa Bwana wa majeshi atatawala katika mlima wa Sayuni, na katika Yerusalemu, na mbele ya wazee wake kwa utukufu.

Bwana anakuja katika Utukufu wake;

Nabii Isaya anatabiri kuhusu hasira ya Mungu juu ya watu wasiomtii. Anaonesha dunia iliyojaa uovu, watu wamelemewa na mizigo ya dhambi inayowalemea, wanaishi upotevuni. Katika mstari wa 21 Isaya anakazia kuwa adhabu ya Bwana ipo kwa watu wote wasiomtii. Isaya alikuwa anaonesha jinsi Mungu anavyoichukia dhambi.

Sisi leo neno la Mungu linatujia moja kwa moja, kwamba Yesu atarudi hivyo tujiandae kumpokea. Tunajiandaa kwa kudumu katika utume kama tulivyoitwa tukimwamini na kumfuata. Tuziepuke dhambi na mazingira yake. Lakini zaidi tutubu dhambi mioyo yetu iwe safi, maana Bwana anakuja katika Utukufu wake.

Siku njema.