Event Date: 
04-04-2022

Siku ya Jumamosi tarehe 2 Aprili 2022 imefanyika ibada ya wazee katika Usharika wa Kanisa Kuu Azana Front Cathedral, jijini Dar es Salaam. Ibada kama hii huwa inafanyika baada ya kipindi maalum ili kuwapa fursa wazee ambao mara nyingi hushindwa kufika kanisani kutokana na sababu mbalimbali hususani zinazotokana na umri wao kuwa mkubwa.

Mwaka huu 2022, ibada imewaleta wazee wa usharika pamoja na kushiriki ibada kanisani wakiwa wamesindikizwa na wasaidizi na ndugu zao wa karibu. Wazee wamepata fursa ya kubadilishana mawazo, kushiriki shughuli mbalimbali za ibada kama kushiriki chakula cha Bwana, kushiriki kuimba ritrugia pamoja nyimbo mbalimbali.

Akizungumza katika ibada hiyo Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amewapongeza wazee walioweza kushiriki ibada na kuwaomba ndugu na jamaa wanaoishi na wazee hao kutosita kuwaleta kanisani wazee wao pindi fursa za ibada ya aiana hiyo zinapojitokeza.

Tunamshukuru Mungu aliyetuwezesha siku ya leo kuwa na Ibada ya Wazee hapa Usharikani. Mungu azidi kuwapa nguvu na afya zaidi wazee wetu wote walioweza kufika na ambao hawajaweza kufika katika Ibada hii ya siku ya leo,” amesema Mchungaji Lwiza.

Mara baada ya ibada kumalizika wazee walipata fursa ya kukaa pamoja na kupata chai iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yao huku wakibadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali ya kanisa na jamii kwa ujumla.

Aidha, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kanisa Kuu Azania Front Cathedral, Mchungaji Charles Mzinga alipata nafasi ya kupita na kuwasalimu wazee katika meza zao walizokuwa wameketi wakinywa chai.

Matukio tofauti katika picha

Wazee wakifuatilia mwendendo wa ibada kupitia vitabu vyao

Wazee wakishiriki meza ya Bwana

Wazee wakishiriki meza ya Bwana

Wazee wakishiriki meza ya Bwana

Wazee wakishiriki meza ya Bwana 

Wazee wakishiriki meza ya Bwana

Mchungaji Charles Mzinga akisalimiana na kuteta na wazee 

Wazee wakipata kifungua kinywa (chai) kanisani mara baada ya ibada

Mchungaji Charles Mzinga akisalimiana na kuteta na wazee 

Picha zaidi tembeleaAZF Ibada ya Wazee 2022