Date: 
18-06-2019
Reading: 
Exodus 33:12-17 (Kutoka 33:12-17)

TUESDAY 18TH JUNE 2019 MORNING                                         

Exodus 33:12-17 New International Version (NIV)

Moses and the Glory of the Lord

12 Moses said to the Lord, “You have been telling me, ‘Lead these people,’ but you have not let me know whom you will send with me. You have said, ‘I know you by name and you have found favor with me.’ 13 If you are pleased with me, teach me your ways so I may know you and continue to find favor with you. Remember that this nation is your people.”

14 The Lord replied, “My Presence will go with you, and I will give you rest.”

15 Then Moses said to him, “If your Presence does not go with us, do not send us up from here. 16 How will anyone know that you are pleased with me and with your people unless you go with us? What else will distinguish me and your people from all the other people on the face of the earth?”

17 And the Lord said to Moses, “I will do the very thing you have asked, because I am pleased with you and I know you by name.”

Moses talked to God face to face. God was pleased with Moses and granted his request. God promised to be with Moses and to help him as he lead the nation of Israel.

We Christians have the Holy Spirit in our hearts. The Holy Spirit will lead and guide us if we listen to Him.

JUMANNE 18TH JUNI 2019 ASUBUHI                                                   

KUTOKA 33:12-17

12 Musa akamwambia Bwana, Angalia, wewe waniambia, Wachukue watu hawa; nawe hukunijulisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Walakini umesema, Nakujua jina lako, nawe umepata neema mbele zangu. 
13 Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako. 
14 Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha. 
15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. 
16 Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi? 
17 Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 

Musa alikuwa na neema kuongea na Mungu uso kwa uso. Mungu alifurahi mwenendo wa Musa. Mungu alimsikiliza Musa na aliitikia maombi yake. Mungu aliahidi kuwa na Musa na kumsaidia kuongoza Wanaisraeli.

Sisi Wakristo tumepewa Roho Mtakatifu kuishi ndani yetu.  Tukimtii Roho Mtakatifu atatusaidia na kutuongoza katika maisha yetu.