Date: 
02-06-2022
Reading: 
Danieli 9:4-9

Alhamisi asubuhi 02.06.2022

Danieli 9:4-9

4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;

5 tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako;

6 wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.

7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.

8 Ee Bwana, kwetu sisi kuna haya ya uso, kwa wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi.

9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi;

Sikia kuomba kwetu;

Baada ya Danieli kuona Taifa la Mungu limetenda dhambi na kumkosea, anaomba rehema ya Mungu akifanya toba. Anakiri hawakumsikiliza Mungu kama kiongozi wao, akiomba haki ya Mungu iwe juu yao wasiangamie.

Nabii Danieli anatufundisha kufanya toba tunapoomba. Toba hutufanya tutakaswe mioyo yetu, ndipo tumwendee Bwana tukimpa haja zetu. Hakuna maisha ya imani bila sala yenye toba.

Siku njema.