Date: 
14-02-2022
Reading: 
Daniel 4:28-33

Jumatatu asubuhi tarehe 14.01.2022

Danieli 4:28-33

28 Hayo yote yakampata mfalme Nebukadreza.

29 Baada ya miezi kumi na miwili, alikuwa akitembea ndani ya jumba la kifalme katika Babeli.

30 Mfalme akanena, akasema, Mji huu sio Babeli mkubwa nilioujenga mimi, uwe kao langu la kifalme, kwa uwezo wa nguvu zangu, ili uwe utukufu wa enzi yangu?

31 Hata neno lile lilipokuwa katika kinywa cha mfalme, sauti ilikuja kutoka mbinguni, ikisema, Ee mfalme Nebukadreza, maneno haya unaambiwa wewe; Ufalme huu umeondoka kwako.

32 Nawe utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni; utalishwa majani kama ng'ombe, na nyakati saba zitapita juu yako, hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote.

33 Saa iyo hiyo jambo hilo likatimizwa, likampata Nebukadreza; alifukuzwa mbali na wanadamu, akala majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa maji kwa umande wa mbinguni, hata nywele zake zikakua, zikawa kama manyoya ya tai, na kucha zake kama kucha za ndege.

Tunaokolewa kwa neema;

Mfalme Nebuchadnezzar baada ya kustarehe katika ufalme wake aliota ndoto ambayo ilimtia hofu, akaita waganga na wachawi wote walioshindwa kumsaidia kutafsiri ndoto. Ndipo somo la asubuhi hii tunamuona mfalme akipewa ujumbe na Mungu kuwa angeondolewa kwenye jumba la kifalme, na kuishi porini akila nyasi. Kweli ilitokea! 

Wokovu tuliopewa na Mungu na maisha tuliyo nayo yasitufanye kusahau kuwa Bwana ndiye mpaji. Nebukadreza aliambiwa angeadhibiwa hadi pale ambapo angetambua kuwa mmiliki wa dunia na ufalme ni Mungu. Nasi ili tusiadhibiwe, tutambue kuwa tumepewa vyote na Bwana kwa neema.

Nakutakia wiki njema yenye neema.