Uzinduzi wa Kinanda (Pipe Organ) na Shukrani ya Chaplain Mzinga

Jumapili tarehe 21/01/2018 Usharika wa Azaniafront ulishuhudia matukio 2 muhimu katika ibada ya Kiswahili ya saa 3:30 asubuhi. La kwanza lilikuwa tukio la kihistoria la uzinduzi wa kinanda kipya kikumbwa (Pipe Organ) chenye hadhi ya kanisa kuu. Uzinduzi huo ulifanywa na Askofu Dr Alex Malasusa, akisaidiwa na Dean Lwiza. Aidha alikuwepo Mch Chuwa na Mchungaji mgeni Gehard Richter kutoka chama cha Biblia cha Lipsig, Ujerumani, ambaye alitoa mahubiri. Mch Richter aliwahi pia kuwa Mchungaji wa KKKT Mto wa Mmbu kwa muda mrefu huko nyuma na msemaji mzuri wa lugha ya Kimaasai.