JUMATANO TAREHE 15 SEPTEMBA 2021, ASUBUHI.
2 Wakorintho 1:3-7
3 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
5 Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.
6 Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
7 Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
Mungu hujishughulisha na mambo yetu;
Mtume Paulo anaeleza na kushukuru juu ya faraja itokayo kwa Mungu katika hali ya kila aina. Paulo anakiri kupata faraja baada ya dhiki katika utume wake;
2 Wakorintho 1:8
8 Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi.
Mtume Paulo anatufundisha kuwa faraja ya kweli hutoka kwa Mungu. Katika hali yoyote ya mateso, shida, dhiki, njaa, ugonjwa, kupungukiwa n.k tukimtegemea Mungu hutufariji.
Mioyo yetu imuelekee yeye Bwana, ili atufariji katika hali zote, maana yeye hujishughulisha na mambo yetu.
Siku njema.
WEDNESDAY 15TH SEPTEMBER 2021, MORNING
2 Corinthians 1:3-7
3 Praise be to the God and Father of our Lord Jesus Christ, the Father of compassion and the God of all comfort, 4 who comforts us in all our troubles, so that we can comfort those in any trouble with the comfort we ourselves receive from God. 5 For just as we share abundantly in the sufferings of Christ, so also our comfort abounds through Christ. 6 If we are distressed, it is for your comfort and salvation; if we are comforted, it is for your comfort, which produces in you patient endurance of the same sufferings we suffer. 7 And our hope for you is firm, because we know that just as you share in our sufferings, so also you share in our comfort.
God is concerned with our affairs;
The apostle Paul explains and appreciates the comfort that God gives in every situation. Paul confesses to finding comfort after tribulation in his mission;
2 Corinthians 1: 8
8 For we do not wish you to be ignorant, brethren, as to our tribulation which happened [to us] in Asia, that we were excessively pressed beyond [our] power, so as to despair even of living.
The apostle Paul teaches us that true comfort comes from God. In any situation of suffering, trouble, distress, hunger, sickness, deprivation etc. if we rely on God we are comforted.
May our hearts be turned to the Lord, for he will comfort us in every way, for he cares for us.
Good day.