Date: 
08-06-2022
Reading: 
1Wakorintho 2:13-16

Jumatano asubuhi tarehe 8.06.2022

1 Wakorintho 2:13-16

13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
 
14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 
15 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
 
16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Roho Mtakatifu njoo kwetu;

Mtume Paulo anawaandikia Wakorintho kuwa Roho Mtakatifu ndiye huwezesha waaminio kunena vema. Paulo anaonesha kuwa aaminiye huyatambua mambo ya Rohoni, tofauti na asiyeamini ambaye huona ni upuuzi.

Mtume Paulo anatukumbusha kuwa maneno tuyasemayo, mawazo na matendo yetu ni muhimu yakawa mema kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Kama tulivyompokea Kristo, vivyo hivyo tudumu katika yeye tukifanya yote kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Siku njema.