Date: 
09-06-2022
Reading: 
1Wakorintho 14:1-5

Alhamisi asubuhi tarehe 09.06.2022

1 Wakorintho 14:1-5

1 Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.

2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

3 Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.

4 Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.

5 Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

Roho Mtakatifu njoo kwetu;

Ni ujumbe wa Mtume Paulo kuhusu kunena kwa lugha, kwamba anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake, bali ahutubuye hulijenga Kanisa la Mungu. Muktadha wa Mtume Paulo hapa ni kuhubiri (kuhutubu) tukiongozwa na Roho Mtakatifu maana tutasema yanayostahili kwa utukufu wa Mungu.

Ni muhimu hapa tukajihoji, kama katika kazi zetu tunaongozwa na Roho Mtakatifu. Kama hatuongozwi na Roho, kamwe hatulijengi Kanisa la Mungu. Na kama hatulijengi Kanisa la Mungu, kazi yetu ni bure. Uko tayari kazi yako iwe bure? Bila shaka hapana. Basi mtumikie Mungu ukiongozwa na Roho Mtakatifu.

Siku njema.