Date: 
22-03-2023
Reading: 
1Wakorintho 11:17-22

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 22.03.2023

1 Wakorintho 11:17-22

17 Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara.

18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;

19 kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.

20 Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana;

21 kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.

22 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

Yesu ni chakula cha uzima;

Mtume Paulo anawaonya Wakorintho juu ya kukusanyika kwao ambako hakumpi Mungu Utukufu, yaani hawakusanyiki katika Bwana. Paulo alihuzunika maana watu wa Korintho walikuwa hawakusanyiki pamoja na kuumega mkate, na hata walipokula kila mmoja alikula 

peke yake alivyojisikia. Hawakuumega mkate na divai katika ukumbusho wa Kristo.

Ujumbe wa Mtume Paulo kwa Kanisa la Korintho ulikuwa ni kukaa pamoja kama kundi la waaminio na kuumega mkate katika ukumbusho wa Kristo. Alikuwa anaonesha umuhimu wa chakula cha Bwana, kama mwili na damu ya Kristo kwa uzima wa milele. Kwa njia hii, tunaalikwa kukaa pamoja kama kundi la Kristo, tukishiriki pamoja kuumega mkate na divai katika yeye. Tukishiriki meza takatifu inavyostahili Yesu hukaa ndani yetu siku zote.

Siku njema.

Heri Buberwa