Hii ni Kwaresma
Jumatatu asubuhi tarehe 20.03.2023
1 Wakorintho 10:1-11
1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6 Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.
7 Wala msiwe waabudu sanamu, kama wengine wao walivyokuwa; kama ilivyoandikwa, Watu waliketi kula na kunywa, kisha wakasimama wacheze.
8 Wala msifanye uasherati, kama wengine wao walivyofanya, wakaanguka siku moja watu ishirini na tatu elfu.
9 Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakaharibiwa na nyoka.
10 Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakaharibiwa na mharabu.
11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
Yesu ni chakula cha uzima;
Mtume Paulo anawaandikia Wakorintho akirejea historia jinsi Israeli walivyotembea jangwani wakila chakula na kunywa kwa msaada Bwana. Lakini bado wengi Mungu hakupendezwa nao, wakangamia jangwani. Yaani walikula mana halafu bado wakatamani mambo mabaya. Paulo anasema mambo haya yameandikwa kutuonya sisi tusiwe kama wao, yaani kutamani mabaya halafu tukaangamia.
Sisi leo tunaishi kwa msaada wa Bwana. Uhai tulio nao na mafanikio yetu ni kwa msaada wa Bwana. Katika yote hayo tusiige mabaya tukaangamia, mfano; tusinung'unike kama Israeli walivyonung'unika wakaangamia, tusimjarihu Bwana kama Israeli walivyomjaribu wakaharibiwa na nyoka. Tumwamini Yesu aliye chakula cha uzima, yaani Mwokozi wa ulimwengu ili tuokolewe katika yeye na kuurithi uzima wa milele.
Nakutakia wiki njema.
Heri Buberwa