Date: 
22-02-2022
Reading: 
1Petro 1:24-25

Jumanne asubuhi tarehe 22.02.2022

1 Petro 1:24-25

24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;

25 Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.

Neno la Mungu lina nguvu;

Petro anaonesha ukuu wa neno la Mungu, pale anapotoa mfano wa mwili akiufananisha na majani yawezayo kukauka na maua yake kuanguka. Yaani pamoja na kuipenda miili yetu, na kwa jinsi tunavyoihudumia, bado miili yetu huondoka katika ulimwengu huu. Tofauti na neno la Mungu ambalo ladumu milele.

Petro anatukumbusha kuwa neno la Mungu hudumu milele. Tusifananishe wala kulinganisha neno la Mungu na kitu chochote. Neno la Mungu ni Yesu mwenyewe ambaye halinganishwi! Lishike neno linalohubiriwa kwako, kwa maisha ya sasa na baadaye.

Siku njema.