Date: 
29-07-2022
Reading: 
1 Yohana 3:13-16

Ijumaa asubuhi tarehe 29.07.2022

1 Yohana 3:13-16

[13]Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia.

[14]Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.

[15]Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

[16]Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.

Amri mpya nawapa; Mpendane 

Yohana anaiona nafasi ya upendo kama amri kuu, hivyo kulisihi Kanisa kupendana kwa dhati. Yohana anasema kuwa asiyependa akaa katika mauti na mwenye chuki ni muuaji asiye na uzima wa milele, hivyo chuki haifai.

Itatufaa nini tutumike miaka yote halafu tuukose uzima wa milele kwa sababu ya kutopendana? 

Chuki inatusaidia nini?

Asubuhi hii nakusihi tutafakari kama njia zetu ni sahihi katika kupendana, na tuombe neema ya Mungu tudumu pendoni, ili kwa pamoja tuurithi uzima wa milele.

Siku njema.