Date: 
11-01-2022
Reading: 
1 Wakorintho 15:29-34

Jumanne asubuhi tarehe 11.01.2022

1 Wakorintho 15:29-34

29 Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?

30 Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa?

31 Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku.

32 Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa.

33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

34 Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

Wabatizwao ndio wana wa Mungu;

Mtume Paulo anawaandikia waKorintho kuhusu uhusiano wa ubatizo na kufa, kuwa tukibatizwa katika Kristo, tunakufa katika Kristo, na tutafufuliwa katika Kristo Yesu. 

Kuhusu jambo hili, Mtume Paulo aliwahi kuwaandikia Warumi;

Warumi 6:3-4

3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
 
4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.

Basi fahamu ya kuwa kwa njia ya ubatizo, sisi tumekuwa watoto wa Mungu. Tukiuishi ubatizo wetu tunaenenda katika upya wa uzima katika maisha ya ufuasi, na mwisho tutakufa na kufufuka katika Kristo.

Siku njema.