Date: 
13-12-2021
Reading: 
Zekaria 4:7-14 (Zechariah)

Jumatatu asubuhi, tarehe 13.12.2021

Zekaria 4:7-14

7 Nani wewe, Ee mlima mkubwa? Mbele ya Zerubabeli utakuwa nchi tambarare; naye atalileta lile jiwe la kuwekwa juu kabisa pamoja na vigelegele vya, Neema, neema, ilikalie.

8 Tena neno la Bwana likanijia, kusema,

9 Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwenu.

10 Maana ni nani aliyeidharau siku ya mambo madogo? Kwa kuwa watafurahi, nao wataiona timazi katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote.

11 Ndipo nikajibu, nikamwambia, Ni nini mizeituni hii miwili iliyo upande wa kuume wa kinara cha taa kile na upande wake wa kushoto?

12 Nami nikajibu mara ya pili, nikamwuliza, Ni nini haya matawi mawili ya mizeituni, ambayo kwa njia ya ile mifereji miwili ya dhahabu hutoa mafuta yao?

13 Akanijibu, akasema, Hujui hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu.

14 Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili wa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.

 

Itengenezeni njia ya Bwana;

Kupitia nabii Zekaria, Bwana anatangaza ukuu wake juu ya vitu vyote. Milki yote ni yake, ambaye atarudi kwa ufufuo na uzima wa milele.

Huyu ndiye Kristo, ambaye tunakumbushwa kusafisha mioyo yetu ili aishi kwetu. Yesu  akikaa ndani ya mioyo yetu tutakuwa safi, tayari kumpokea  arudipo mara ya pili.

Uwe na wiki njema.


Monday morning, 13th December 2021

Zechariah 4:7-14

Then the word of the Lord Almighty came to me: “Ask all the people of the land and the priests, ‘When you fasted and mourned in the fifth and seventh months for the past seventy years, was it really for me that you fasted? And when you were eating and drinking, were you not just feasting for yourselves? Are these not the words the Lord proclaimed through the earlier prophets when Jerusalem and its surrounding towns were at rest and prosperous, and the Negev and the western foothills were settled?’”

And the word of the Lord came again to Zechariah: “This is what the Lord Almighty said: ‘Administer true justice; show mercy and compassion to one another. 10 Do not oppress the widow or the fatherless, the foreigner or the poor. Do not plot evil against each other.’

11 “But they refused to pay attention; stubbornly they turned their backs and covered their ears. 12 They made their hearts as hard as flint and would not listen to the law or to the words that the Lord Almighty had sent by his Spirit through the earlier prophets. So the Lord Almighty was very angry.

13 “‘When I called, they did not listen; so when they called, I would not listen,’ says the Lord Almighty. 14 ‘I scattered them with a whirlwind among all the nations, where they were strangers. The land they left behind them was so desolate that no one traveled through it. This is how they made the pleasant land desolate.’”

Read full chapter

 

Prepare the way of the Lord;

Through the prophet Zechariah, the Lord declares His greatness over all things. All possessions belong to Him, who will return in the resurrection and eternal life.

This is the Christ, whom we are reminded to cleanse our hearts so that he might live in us. If Jesus abides in our hearts we will be clean, ready to receive Him when He returns a second time.

Have a great week.