MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 09 FEBRUARI, 2025  

SIKU YA BWANA YA MWISHO KATIKA MAJIRA YA UFUNUO

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI  

UTUKUFU WA MWANA WA MUNGU

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Mgeni aliotufikia kwa cheti ni Emmanuel Hiyob Metili toka Usharika wa Ilboru Mtaa wa kati Arusha. Amekuja kwenye Matibabu.  

3. Matoleo ya Tarehe 02/02/2025

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Mahudhurio ya ibada zote3 za  tarehe 02/02/2025 ilikuwa ni washarika 822. 

5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV.

6. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=. 

7. Leo tarehe 09/02/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika Karibunini.  

8. NDOA: Hakuna Ndoa za Washarika

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa Matangazo karibu na Duka letu la Vitabu.

9. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Keneth Zebedayo 
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Nyamajeje Buchanagandi
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Nisile Mollel
  • Kinondoni: Kwa Prof. Na Bibi Kulaba
  • Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.

10. Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tuna kurasa Facebook na Instagram

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili  

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.