DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI
MATANGAZO YA USHARIKA
TAREHE 02 MACHI, 2025
SIKU YA BWANA YA 7 KABLA YA PASAKA
NENO LINALOTUONGOZA NI
YESU ANAYAENDEA MATESO YERUSALEMU
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna Mgeni aliyetufikia na cheti.
3. Matoleo ya Tarehe 23/02/2025
Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Lipa namba M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Mahudhurio ya ibada ya tarehe 23/02/2025 ilikuwa ni washarika 809. Sunday School 98.
5. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. Vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 mchana. Alhamisi saa 11.00 jioni tuna kipindi cha Maombi na Maombezi, ambapo tunajifunza neno la Mungu na kupata muda wa kutosha wa maombi. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front Cathedral.
6. Leo tarehe 02/03/2025 tutamtolea Mungu fungu la kumi. Washarika karibu.
7. Jumatano ijayo tarehe 05/03/2025 saa 11.00 jioni kutakuwa na ibada ya majivu. Kwaya zote zitahudumu. Wazee wote watakuwa zamu
8. Kitenge chetu kipya cha Kiharaka kinapatikana hapo nje na kwenye duka letu la vitabu kwa bei ya Tsh. 40,000/=.
9. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kwa matukio ya mwezi wa tatu.
10. Ijumaa ijayo tarehe 07/03/2025 ni siku ya maombi ya dunia yatakayofanyika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 3.00 asubuhi. Hivyo kwa wale ambao wataanzia hapa Kanisani safari itaanza saa moja kamili asubuhi
11. Jumapili ijayo tarehe 09/03/2025 siku ya Wanawake kuongoza ibada Sharika na Mitaa yote ngazi ya Dayosisi. Hivyo siku hiyo Wanawake wataongoza ibada zote.
12. Jumatano ijayo tarehe 12/03/2025 siku ya kurudia maombi katika ibada. Siku hiyo pia wanawake wataongoza ibada.
13. IBADA ZA NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mzee Evatt Kuzilwa
- Upanga: Kwa Bwana na Bibi Mbwilo, mtaa wa Isimani no 322
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bwana na Bibi Christopher Kivulege
- Oysterbay/Masaki: Kwa Mama Vicky Katikaza
- Kinondoni: Kwa Bwana na Bibi Danford Mariki.
- Mjini kati: Watafanyia hapa kanisani saa 1.00 asubuhi.
- Kwa habari na taarifa nyingine, tembelea tovuti yetu ya Azania front.org, pia tupo Facebook na Instagram.
14. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza
Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.