Hii ni Kwaresma
Alhamisi asubuhi 31.03.2022
Zaburi 42:1-6
1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.
4 Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
5 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
6 Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.
Yesu ni mkate wa uzima;
Zaburi ya asubuhi hii inamuita Bwana kama tegemeo la maisha ya waaminio katika maisha ya kila siku. Ni shauku ya mtu mwenye kuhitaji kumwona Bwana. Ni mtu aliyetoa machozi kumtafuta Mungu katika njia zake.
Ni wazi kuwa hakuna awezaye kuyamudu maisha haya bila msaada wa nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yetu. Tunayo shauku ya kumwona Yesu? Tunaalikwa kwenda kwa Yesu ili kuponywa roho zetu, kwa ajili ya sasa na uzima wa Ulimwengu ujao.
Siku njema.