Date: 
22-10-2021
Reading: 
Zaburi 18:1-3 (Psalm)

IJUMAA TAREHE 22 OKTOBA 2021, ASUBUHI.

Zaburi 18:1-3

1 Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana;

2 BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,

Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,

Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.

3 Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa,

Hivyo nitaokoka na adui zangu.

Njia ya ufalme wa Mungu;

Somo la asubuhi ya leo ni wimbo wa Daudi akitoa shukrani kwa Mungu, baada ya yeye Daudi kuwashinda adui zake. Daudi alimtegemea Bwana, na Bwana akamwokoa na mkono wa adui zake.

Katika kuutafuta ufalme wa Mungu, ni Mungu tu anaweza kutuongoza na kutushindia. Mungu hawezi kutuongoza kama hatufuati neno lake, kufanya ibada ya kweli, toba na sala katika njia ya ufuasi. Tukimtegemea yeye tutashinda na kuuingia katika ufalme wa Mungu.

Siku njema.


FRIDAY 22ND OCTOBER 2021, MORNING

Psalm 18:1-3

For the director of music. Of David the servant of the Lord. He sang to the Lord the words of this song when the Lord delivered him from the hand of all his enemies and from the hand of Saul. He said:

I love you, Lord, my strength.

The Lord is my rock, my fortress and my deliverer;
    my God is my rock, in whom I take refuge,
    my shield[b] and the horn[c] of my salvation, my stronghold.

I called to the Lord, who is worthy of praise,
    and I have been saved from my enemies.

Read full chapter

Footnotes

  1. Psalm 18:1 In Hebrew texts 18:1-50 is numbered 18:2-51.
  2. Psalm 18:2 Or sovereign
  3. Psalm 18:2 Horn here symbolizes strength.

The way to the kingdom of God;

This morning's lesson is a song of David giving thanks to God, after David defeated his enemies. David trusted in the Lord, and the Lord delivered him from the hand of his enemies.

In seeking the kingdom of God, only God can guide and overcome for us. God cannot lead us if we do not follow His word, practice true worship, repentance, and prayer in the path of discipleship. If we trust in Him we will overcome and enter the kingdom of God.

Good day.