Date: 
04-08-2022
Reading: 
Zaburi 118:10-14

Alhamisi asubuhi 04.08.2022

Zaburi 118:10-14

[10]Mataifa yote walinizunguka; 

Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.

[11]Walinizunguka, naam, walinizunguka; 

Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.

[12]Walinizunguka kama nyuki, 

Walizimika kama moto wa miibani; 

Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.

[13]Ulinisukuma sana ili nianguke; 

Lakini BWANA akanisaidia.

[14]BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, 

Naye amekuwa wokovu wangu.

Mungu amejaa neema inayotuwezesha;

Zaburi ya 118 ni wimbo wa ushindi wa Israeli unaomshukuru Mungu kwa kuwa mwema, mwenye fadhili kati ya watu. Katika wimbo huu Israeli wanaonesha walivyozingirwa, lakini Bwana akawa nao, akawaokoa. Wanaonesha ukuu wa Bwana wakiahidi kumtumikia siku zote.

Maisha yetu ya ufuasi yamejaa vikwazo vingi, ambavyo kuvivuka au kuvishinda siyo nguvu zetu zinaweza, bali kwa neema ya Mungu. Tukilijua hilo tuendelee kumshukuru na kumtegemea yeye atujaliaye ushindi katika safari yetu ya Imani. Tuendelee kumtumikia Bwana, tukimshukuru kama Israeli walivyofanya;

Zaburi 118:29

[29]Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Siku njema.