Date: 
07-06-2021
Reading: 
Yohana 7:1-9 (John 7:1-9)

JUMATATU TAREHE 7 JUNI 2021, ASUBUHI

Yohana 7:1-9

1 Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Uyahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.
Na sikukuu ya Wayahudi, Sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.
Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Uyahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.
Kwa maana hakuna mtu afanyaye neno kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu.
Maana hata nduguze hawakumwamini.
Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote upo.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.
Kweeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sikwei bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa haujatimia wakati wangu.
Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alikaa vivi hivi huko Galilaya.

Mungu au ulimwengu;

Yesu alikuwa anafanya kazi katika mazingira ya kukataliwa. Hata ndugu zake hawakumwamini. Hata alipokwea kwa ajili ya sikukuu ya vibanda, alikwea kwa siri (mst 10) maana Wayahudi walitaka kumwua.

Waliomkataa Yesu ni alama ya wale ambao bado hawamwamini Yesu. Kwa leo, hata kutolitii neno la Mungu  ni kumkataa Yesu. Msingi wa Kanisa ni neno la Mungu, hivyo kulikataa neno la Mungu ni kumkataa Yesu, Mungu mwenyewe.

Tunapomkubali Yesu tunakuwa kwa Mungu, bali tukimkataa tunakuwa kwa Ulimwengu. Hatma yetu itategemea tuko kwa nani.

Tunaitwa kumpokea na kumkubali Yesu. Kumkubali ni kumwamini na kulishika neno lake, katika maisha ya wokovu. Tujihoji, kama kweli tumemkubali Yesu na kuchukua hatua stahiki. Nakutakia wiki njema.


MONDAY 7TH JUNE 2021, MORNING

John 7:1-9 [NIV]

1 After this, Jesus went around in Galilee. He did not want[a] to go about in Judea because the Jewish leaders there were looking for a way to kill him. But when the Jewish Festival of Tabernacles was near, Jesus’ brothers said to him, “Leave Galilee and go to Judea, so that your disciples there may see the works you do. No one who wants to become a public figure acts in secret. Since you are doing these things, show yourself to the world.” For even his own brothers did not believe in him.

Therefore Jesus told them, “My time is not yet here; for you any time will do. The world cannot hate you, but it hates me because I testify that its works are evil. You go to the festival. I am not[b] going up to this festival, because my time has not yet fully come.” After he had said this, he stayed in Galilee.

Read full chapter

Footnotes

  1. John 7:1 Some manuscripts not have authority
  2. John 7:8 Some manuscripts not yet

God or the universe;

Jesus was working in a context of rejection. Even his brothers did not believe him. Even when he ascended for the feast of tabernacles, he ascended in secret (v. 10) because the Jews sought to kill him.

Those who rejected Jesus are the mark of those who still do not believe in Jesus. Today, even disobeying God's word is a rejection of Jesus. The foundation of the Church is the word of God, so to reject the word of God is to reject Jesus, God Himself.

When we accept Jesus we belong to God, but if we reject Him we belong to the world. Our destiny will depend on who we are.

We are called to receive and accept Jesus. Accepting Him is believing in Him and keeping His word, in the life of salvation. Let us question ourselves, whether we have truly accepted Jesus and taken appropriate action. I wish you a good week.