Date: 
08-12-2021
Reading: 
Yohana 3:31-32

Hii ni Advent 

Jumatano asubuhi tarehe 08.12.2021

Yohana 3:31-32

[31]Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.

[32]Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake.

Bwana anakuja katika Ufalme wake;

Yohana Mbatizaji anaendelea kutangaza ujio wa Yesu ajaye, kuwa yuko juu ya yote. Ukiendelea kusoma unaona Yohana akikazia kuwa Yesu anatoka mbinguni kwa baba, ushuhuda wake ni wa kweli, na yeyote amwaminiye anao uzima wa milele.

Sauti ya Yohana ilitangaza ujio wa Yesu. Nasi leo tunakumbushwa ujio wa Yesu kwa mara ya pili, ambapo wote wamwaminio wataurithi uzima wa milele kama Yohana alivyoshuhudia;

Yohana 3:36

[36]Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Mwamini Yesu uwe na uzima wa milele.

Siku njema.