Date: 
07-09-2022
Reading: 
Yakobo 2:10-12

Jumatano asubuhi 07.09.2022

Yakobo 2:10-12

[10]Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

[11]Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.

[12]Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.

Tutumie vizuri ndimi zetu;

Yakobo anaandika juu ya kuzishika amri za Mungu, akikumbusha kuwa ukikosa juu ya amri moja unakuwa umekosa juu ya zote. Amri zote zimetoka kwa Mungu mmoja, na alizitoa kwa pamoja, kama zinavyofuatana. Kutoka kwa Mungu mmoja ni sababu tosha ya kukosa juu ya moja ikawa kukosa juu ya zote.

Amri mojawapo ni hii;

Kutoka 20:16
[16]Usimshuhudie jirani yako uongo.

Tukishuhudia uongo tunatumia ulimi. Na kwa kuwa tumeshuhudia uongo, tunakuwa tumevunja amri ya Mungu. Kumbuka amri kuu ni upendo. Hivyo kushuhudia uongo ni kukosa upendo, ambayo ni amri kuu.

Usishuhudie uongo.

Siku njema.