Date: 
01-12-2021
Reading: 
Warumi 14:17-19

Jumatano asubuhi tarehe 01.12.2021

Warumi 14:17-19

[17]Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
[18]Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.
[19]Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.

Bwana analijia Kanisa lake;

Ufalme wa Mungu ni kuishi maisha yanayompendeza Mungu tukiepuka uovu. Kumpendeza Mungu ni kufanya yale anayotuagiza kufanya, tukiongozwa na Roho Mtakatifu.

Tukimpendeza Mungu ndipo tunakuwa na haki ya kuurithi uzima wa milele ulioandaliwa kwa ajili yetu. Umejiandaaje?  Chukua hatua ya imani kuuendea uzima wa milele ukiishi kwa kumpendeza Mungu, yaani ukifanya atakayo Mungu.

Siku njema.