Date: 
15-02-2023
Reading: 
Wafilipi 1:12-18

Jumatano asubuhi tarehe 15.02.2023

Wafilipi 1:12-18

12 Lakini, ndugu zangu, nataka mjue ya kuwa mambo yote yaliyonipata yametokea zaidi kwa kuieneza Injili;

13 hata vifungo vyangu vimekuwa dhahiri katika Kristo, miongoni mwa askari, na kwa wengine wote pia.

14 Na wengi wa hao ndugu walio katika Bwana, hali wakapata kuthibitika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kunena neno la Mungu pasipo hofu.

15 Wengine wanahubiri habari za Kristo kwa sababu ya husuda na fitina; na wengine kwa nia njema.

16 Hawa wanamhubiri kwa pendo, wakijua ya kuwa nimewekwa ili niitetee Injili;

17 bali wengine wanamhubiri Kristo kwa fitina, wala si kwa moyo mweupe, wakidhani kuongeza dhiki za kufungwa kwangu.

18 Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo anahubiriwa; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi.

Neno la Mungu lina nguvu;

Mtume Paulo alipitia nyakati ngumu hudumani ikiwemo kufungwa gerezani. Ndiyo maana asubuhi hii tunamsoma akisema kuwa yote yaliyompata ni kwa sababu ya kuieneza Injili. Kwa leo naweza kusema alipitia nyakati ngumu kwa sababu ya kuhubiri neno la Mungu. Anawaita Wafilipi kudumu katika neno la Mungu, lakini wakihubiri neno kwa nia njema, yaani watu wamjue na kumpokea Kristo.

Kwa mujibu wa Paulo, kazi ya Injili siyo nyepesi. Kuhubiri siyo kazi rahisi, pia kuishi kwa kadri ya neno la Mungu siyo rahisi. Lakini neno hilo tukilisikia na kulifanyia kazi, tunaweza kushinda katika nyakati za aina zote tunazozipitia, maana neno la Mungu lina nguvu.

Jumatano njema.

Heri Buberwa