Date: 
28-01-2023
Reading: 
Waefeso 5:6-9

Jumamosi asubuhi tarehe 28.01.2023

Waefeso 6:5-9

[5]Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;

[6]wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;

[7]kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;

[8]mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.

[9]Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.

Yesu anaondoa ubaguzi;

Mtume Paulo anawasihi walio watumwa katika Efeso kuwatii walio Bwana zao kwa unyofu wa moyo. Anawaita kujitambua kama watumwa, hivyo wawe wanyenyekevu kama kumtii Kristo. Anawaambia wasifanye kwa kupendeza watu machoni, bali wafanye kwa kumcha Bwana. 

Paulo pia anawaasa bwana kuwatendea vema watumwa wao kwa upendo wakijua kuwa Bwana ni mmoja aliye juu ambaye hana upendeleo.

Hapa tunafundishwa kutendeana wema sisi kwa sisi, kwa mfano wa Mungu wetu ambaye hana upendeleo. Upendeleo haufai.

Jumamosi njema