Date: 
21-02-2023
Reading: 
Waebrania 2:1-4

Jumanne asubuhi tarehe 21.02.2023

Waebrania 2:1-4

1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.

2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,

3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

Tazameni tunapanda kwenda Yerusalemu;

Mwandishi wa Waraka kwa Waebrania anaandika juu ya kukumbuka habari ya wokovu kama tulivyoisikia na kuipokea. Anakumbusha juu ya neno la Mungu lililotujia kwa njia ya Yesu Kristo kama njia sahihi ya wokovu. Ndiyo maana katika mstari wa tatu anauliza kwamba tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii? Ambao uliletwa na Mungu mwenyewe kwa njia ya kifo cha Kristo?

Ujumbe wa asubuhi ya leo ni kuendelea kukumbuka kwamba Kristo aliiendea njia ya mateso kwa ajili yetu. Tusilisahau hilo.

Tunapokumbuka Yesu kuiendea njia ya mateso, tutafakari njia zetu kama zinaakisi wokovu tulioletewa naye Kristo kwa njia ya kifo chake, maana aliteswa na kufa kwa ajili yetu.

Siku njema.

Heri Buberwa