Date: 
24-11-2021
Reading: 
Waebrania 12:18-24

Jumatano asubuhi 24.11.2021

Waebrania 12:18-24

[18]Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani,

[19]na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine;

[20]maana hawakuweza kustahimili neno lile lililoamriwa, Hata mnyama akiugusa huo mlima atapigwa kwa mawe.

[21]Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.

[22]Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

[23]mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,

[24]na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.

Uzima wa Ulimwengu ujao;

Asubuhi hii tunasoma kuhusu maonyo juu ya walioikataa neema ya Mungu, na kuishi watakavyo. Ni onyo kwa walioshindwa kumudu njia zao, kwa kutomtegemea Yesu. Lakini pamoja na yote, bado Yesu anabaki kuwa mjumbe wa Agano jipya, aliyebeba ujumbe wa wokovu.

Kuikataa neema ya Mungu na kumfuata kwa ukamilifu ni njia ya kuukosa ufalme wa Mungu. Nini unafanya kuliepuka hili? Mungu atakayetupokea uzimani ndiye atupaye neema ya kumfuata kwa ukamilifu. Hivyo usiiache neema hii, ili uufikie uzima wa Ulimwengu ujao.

Nakutakia siku njema.