Event Date: 
14-12-2020

Jumapili ya Tarehe 13/12/2020, Washarika walishuhudia kwaya ya vijana ikizindua album yenye Jina "Hakuna Jina Lingine"  yenye nyimbo 8 katika ibada ya kwanza na ya tatu. Uzinduzi  huo ulifanywa na Chaplain Charles Mzinga aliyekuwa pia akiongoza ibada. Albam hii imekuja baada ya muda mrefu wa Kwaya ya Vijana kutokuwa na kazi mpya. Mweyekiti wa Uinjilisti Mzee S Jengo alisema haya ni matokeo ya mpango mkakati wa miaka minne ambapo mbali na uzinduzi ya album hii, vijana wana mpango wa mradi uchumi katika eneo letu mtaa wa Tabora. 

Chaplain Mzinga akipokea CD kwa uzinduzi.