Umoja wa wanawake KKKT Azania Front waendeleza jadi yao ya kutembelea hospital ya mbalimbali kwa ajili ya kuwaona wagonjwa, jumamosi ya terehe 14 Nov 2015 walifanikiwa kutembelea hospitali ya Ocean Road na kuwapeleka wagojwa zawadi mbalimbali. kila mwaka umoja wa wanawake wa KKKT Azania Front wana utaratibu wa kupeleka misaada mbalimbali katika Hospital ya Ocean Road, Baadhi ya misaada hili huwa ni Sabuni za kuogea na kufulia, Sukari, dawa ya mswaki, miswaki,Mafuta ya kujipaka, Nguo na vitu vingine. Mchungaji Charles Mzinga aliungana na wanawake wa Azania Front na kuwasihi waendelee na moyo huo huo wa kujitolea kidogo walicho nacho Mungu atawabariki. Pia aliombea zawadi na kuwaombea wanawake hao waendelee kumshika na kumtumikia Mungu kwa umoja wao Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Azania Front Mama Apaisaria Kilewo na Viongozi wenzake waliongoza kundi la wanawake wa Azania front kwenda hospital ya Ocean Road kwa ajili ya kutoa misaada na kuwafariji wagonjwa katika hospital hiyo. Misaada hiyo inatolewa na wanawake hao wakishirikiana kikamilifu na washarika wa usharika wa Azania Front, “tuwena mazoea ya kumtolea mungu kwa njia yakuwasaidia wengine bila kuchoka maana mungu ana makusudi yake na ndio maana amekupa pumzi ufanye lile linalompendeza ili mapenzi yake yatimizwe” alieleza mchugaji Charles Mzinga. |
Baadhi ya vitu ambavyo vimeandaliwa kwa ajili ya msaada vikiwa bado havijafugwa.
baadhi ya misaada iliyokusanywa
Baadhi ya nguo ambao ilitolewa na Washarika wa Azania front.
Mama Elly Monyo akipeleka mzigo kwenye gari tayari kwa safari ya uinjilisti katika Hospital ya Ocean Road.
Mama kaale wakishirikina na Dada Upendo kufunga zawadi.
Mama Mavura na mama Kaduri wakielekezana jambo katika ufungaji zawadi za kupeleka hospitali.
Mama Msangi akipaki zawadi akishrikiana na kinamama wenzake.
Mama Stella Sykes akiandaa miswaki kwa ajili ya kupaki kwenye mifuko.
Mama Swai wakijadilina jambo na Mama Bgoya katika kufunga zawadi.
Mchungaji Charles Mzinga akiombea vitu vilivyoandaliwa kwa msaada.
Mchungaji Charles Mzinga akisema neno kwa umoja wa wanawake wa Azania Front.
Mchungaji Mzinga akiwapa moyo wanawake wa Azania front kuendelea na tabia ya kumtumikia mungu kwa njia tofauti kama kuwajali
wagonjwa wasiojiweza.
Mifuko iliyokuwa pakiwa vitu ikiwa tayari tayari.
Mmoja wa kinamama akipanga sabuni kwa ajili ya kuzifungasha.
Mwenyekiti Apaisaria kilewo akitoa maelezo ya safari ya uinjilisti.
Mwenyekiti wa umoja wa kinamama Usharika wa azania front Mama Kilewo akitoa maelekezo.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake Mama Apaisaria Kilewo na wenzake wakiiandaa sabuni.
Parish Worker akuwa nyuma kwenye tukio hili naye alijumuhika ipasavyo kuahakikisha zoezi linakamilika.
ÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂ sukari,dawa ya mswaki,sabuni nk Vilikusanywa na wakina mama wa usharika wa Azania Front kwa ajili ya kuwapelekea misaada wagonjwa katika hospitali ya Ocean road.
Umoja wa ÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂ wanawake wakiiba nyimbo za kumtukuza Mungu kwa kutimia malengo yao.
Umoja wa wanawake wakiwa busy kwa kupanga vitu kwa ajiri ya kuvipeleka Hospital ya ÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂ Ocean Road.
viongozi wa umoja wa wanawake na washarika wengine wakiwa wa Azania Front katika picha wakiimba.
ÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂÂ
wenyekiti wa umoja wa wanawake azania front akisema achache kwa viongozi na Washarika.
Angalia picha zingine hapa