Date: 
11-11-2021
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 17:12-14

Alhamisi asubuhi tarehe 11.11.2021

Ufunuo wa Yohana 17:12-14

[12]Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.

[13]Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.

[14]Hawa watafanya vita na Mwana Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.

Uenyeji wa mbinguni;

Sura ya 17 ya ufunuo imetumia lugha ngumu, lakini Yohana alikuwa anaoneshwa kukoma kwa utawala wa Babeli. Yohana anatumia lugha isiyo nyepesi kuelezea wafalme watakavyoondolewa na Yesu kutawala, maana atawashinda kwa vita. Yeye ndiye Bwana wa maBwana, mfalme wa wafalme.

Hakuna ufalme ambao hautakoma hapa duniani. Yesu pekee ndiye mtawala milele yote. Hivyo mtafute na kumfuata Yesu aliye mtawala wa kudumu, maana ndiye atakayetupokea katika ufalme wake.

Alhamisi njema.