Date: 
13-11-2021
Reading: 
Ufunuo wa Yohana 14:4-7 (Revelations)

JUMAMOSI TAREHE 13 NOVEMBA 2021, ASUBUHI.

Ufunuo wa Yohana 14:4-7

4 Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.

5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.

6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,

7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.

Uenyeji wa mbinguni;

Mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo ni wajibu wake kuishi katika njia za haki, yaani pasipo mawaa. Yohana anafunuliwa kutuhubiria kumcha BWANA,  maana saa ya hukumu inakuja.

Tufahamu ya kuwa tunatakiwa kuishi kwa kumfuata Yesu siku zote kwa utimilifu, kwa msaada  wa Roho Mtakatifu, tukijua kuwa hukumu inakuja, ambapo kila mtu atahukumiwa kwa kadri ya matendo yake.

Siku njema.


SATURDAY 13TH NOVEMBA 2021, MORNING.

Revelations 14:4-7 NIV

These are those who did not defile themselves with women, for they remained virgins. They follow the Lamb wherever he goes. They were purchased from among mankind and offered as first fruits to God and the Lamb. No lie was found in their mouths; they are blameless.

The Three Angels

Then I saw another angel flying in mid-air, and he had the eternal gospel to proclaim to those who live on the earth—to every nation, tribe, language and people. He said in a loud voice, “Fear God and give him glory, because the hour of his judgment has come. Worship him who made the heavens, the earth, the sea and the springs of water.”

Read full chapter

Citizenship of Heaven;

Man is made in the image of God, so it is his responsibility to live in the way of righteousness, that is, without blemish. John is revealed to preach the fear of the Lord, for the hour of judgment is coming.

We know that we must always live by following Jesus fully, with the help of the Holy Spirit, knowing that judgment is coming, in which everyone will be judged according to their deeds.

Good day.