Date: 
19-08-2022
Reading: 
Tito 1:5-9

Ijumaa asubuhi tarehe 19.08.2021

Tito 1:5-9

[5]Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru;

[6]ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.

[7]Maana imempasa askofu

awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu;

[8]bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake;

[9]akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.

Hekima ituingizayo mbinguni;

Mtume Paulo mwanzoni kabisa mwa waraka wake kwa Tito anamwambia jinsi Askofu anavyotakiwa awe. Awe muadilifu, asiyejipenda mwenyewe, mkaribishaji, siyo mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, mwenye mapato ya halali, mwema, mwenye kiasi, na mambo mengine kama hayo. Hakutakiwa kuwa mtu mwenye kulaumika, ili aweze kuwaongoza wengine kwa mfano.

Leo, lugha ya Askofu kwenye waraka huu inaweza kusimama badala ya "mwangalizi". Na kwa ajili ya Kanisa la Mungu, ninaweza kusema ujumbe huu unamhusu yeyote aliyeitwa kuifanya kazi ya Mungu. Tunaitwa kuwa waadilifu, wenye kiasi, wenye kiasi, na sifa nyinginezo kama zilivyo kwenye somo la leo asubuhi (soma tena hapo juu). Ishi maisha yenye uchaji, ili Mungu atukuzwe kupitia wewe. Siku njema.