Date: 
03-11-2016
Reading: 
THURSDAY 3rd NOVEMBER 2016 MORNING

THURSDAY  3rd  NOVEMBER 2016 MORNING                              

John 5:30-37 New International Version (NIV)

30 By myself I can do nothing; I judge only as I hear, and my judgment is just, for I seek not to please myself but him who sent me.

Testimonies About Jesus

31 “If I testify about myself, my testimony is not true. 32 There is another who testifies in my favor, and I know that his testimony about me is true.

33 “You have sent to John and he has testified to the truth. 34 Not that I accept human testimony; but I mention it that you may be saved.35 John was a lamp that burned and gave light, and you chose for a time to enjoy his light.

36 “I have testimony weightier than that of John. For the works that the Father has given me to finish—the very works that I am doing—testify that the Father has sent me. 37 And the Father who sent me has himself testified concerning me. You have never heard his voice nor seen his form,

There is plenty of evidence that Jesus Christ is God’s son. Let us read the Testimony in the Bible. Let us trust in Jesus as our Lord and savior. Let us commit our lives to Him today and every day.

 

ALHAMISI TAREHE 3 NOVEMBA 2016 ASUBUHI                        

YOHANA 5:30-37

30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka. 
31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli. 
32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli. 
33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli. 
34 Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka. 
35 Yeye alikuwa taa iwakayo na kung'aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda. 
36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma. 
37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona. 

Kuna ushuhuda wa kutosha kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Tumwamini leo . Tumtegemee leo na siku zote za maisha yetu.